Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 14 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Juni 2027
Jumatatu · Juma la 11 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 11 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo. 2Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu. 3Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya. 4Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha, 5kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa, 6katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi. 7Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto. 8Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli. 9Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa. 10Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
Wimbo wa katikati
1Zaburi. Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi. 2Yahwe ameufanya wokovu wake ujulikane; ameidhihirisha haki yake kwa mataifa yote. 3Hukumbuka uaminifu wa agano lake na uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia itauona ushindi wa Mungu wetu. 4Mshangilieni Yahwe, nchi yote; pazeni sauti kwa wimbo, imbeni kwa furaha, na imbeni sifa.
Injili
38Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.' 39Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia. 40Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia. 41Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili. 42Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki