Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 24 Mei
Kalenda ya Kiorthodoksi · 11 Mei (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 24 Mei 2027
Jumatatu · Wiki ya 4 ya Pasaka · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini wa Kikasisi Mokio († karibu 295)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
31Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa. 32Midomo ya wale watendao mema huyajua yanayokubalika, bali kinywa cha waovu, huyajua yanayopotosha. 11:1Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri. 2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima. 3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza. 4Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti. 5Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao. 6Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao. 7Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu. 8Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu. 9Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama. 10Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha. 11Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa. 12Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Alfajiri: Injili
1Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi. 2Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje. 4Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake. 5Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.” 6Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao. 7Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo. 8Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza. 9Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
Waraka
1Kulikuwa na mtu fulani katika mji wa kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia. 2Alikuwa mchamungu na alimwabudu Mungu na nyumba yake yote; alitoa pesa nyingi kwa wayahudi na aliomba kwa Mungu siku zote. 3Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia “Kornelio! 4Kornelio akamwangalia malaika na alikuwa na hofu kubwa sana akasema “Hii ni nini mkuu?” Malaika akamwambia “Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu”. 5Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu mmoja anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro. 6Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.” 7Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka, Kornelio akawaita watumishi wa nyumbani kwake wawili, na askari aliyekuwa akimwabudu Mungu kati ya maaskari waliokuwa wanamtumikia. 8Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa. 9Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba. 10Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono, 11akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne. 12Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani. 13Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule”. 14Lakini Petro akasema “Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu. 15Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili “Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu”. 16Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.
Waraka (Watakatifu)
26Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu. 27Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe. 28Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele. 8:1Sasa jambo ambalo tunasema ni hili: tunaye kuhani mkuu aliyekaa chini katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi Mbinguni. 2Yeye ni mtumishi katika mahali patakatifu, hema la kweli ambalo Bwana ameliweka, siyo mtu yeyote wa kufa.
Injili
56Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake. 57Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, na yeye pia ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele. 59Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu. 60Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?” 61Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza? 62Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla? 63Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima. 64Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti. 65Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba.” 66Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena. 67Yesu akawambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?” 68Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele, 69na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”
Injili (Watakatifu)
14Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki. 15Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba. 16Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni. 17Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza. 18Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa. 19Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Watakatifu wa siku
- Methodio († 885) na Kirilo († 869) Sawa na Mitume, walimu wa Waslavoni
- Rostislav Sawa na Mitume, mwana wa mfalme wa Moravia Kuu (870)
- Mfiadini wa Kikasisi Mikaeli, padri (1920)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, Askofu Mkuu wa Kharkiv (1940)
- Mtakatifu Mtawa Sofronio, mtawa wa faragha wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
- Mfiadini wa Kikasisi Yusufu, Mitropoliti wa Astrakhan (1671)
- Askofu Mtakatifu Nikodemo, Askofu Mkuu wa Serbia (1325)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 11 Mei katika kalenda ya kanisa ni 24 Mei katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki