Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 25 Mei
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Mei (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Mei 2027
Jumanne · Wiki ya 4 ya Pasaka · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Epifani, Askofu wa Kipro (403)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
21Petro akashuka chini kwao na kusema “Mimi ni yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?” 22Wakasema, “Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu wa haki na hupenda kumwabudu Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, ameambiwa na malaika wa Mungu kukutuma ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako.” 23Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja naye, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye. 24Siku iliyofuata walikuja Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu. 25Wakati Petro akiingia ndani, Kornelio akamlaki na kuinama hadi chini kwenye miguu yake kwa kumheshimu. 26Lakini Petro akamwinua na kusema “Simama; mimi mwenyewe pia ni mwanadamu.” 27Wakati Petro akiwa anaongea naye, alienda ndani akakuta watu wamekusanyika pamoja. 28Akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kuwa siyo sheria ya kiyahudi kushirikiana au kutembelewa na mtu ambaye si wa taifa hili. Lakini Mungu amenionesha mimi kuwa sipaswi kumwita mtu yeyote ni najisi au mchafu. 29Na ndiyo maana nimekuja bila kubisha, nilipotumwa kwa ajili ya hiyo. Kwa hiyo niwaulize kwa nini mlitumwa kwa ajili yangu.” 30Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, wakati kama huu nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Nikaona mbele yangu mtu amesimama akiwa na mavazi meupe, 31Akaniambia “Kornelio maombi yako yamesikiwa na Mungu, na zawadi zako kwa masikini zimekuwa ukumbusho mbele za Mungu. 32Kwa hiyo tuma mtu Yafa na akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako, ambaye pia huitwa Petro. ambaye anaishi kwa mtengenezaji wa Ngozi mmoja aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko pembeni mwa bahari. 33Zingatia: Msatri huu, “Naya atakapokuja atasema nanyi,” haumo kwenye maandiko ya kale.
Injili
1Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua. 2Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. 3Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo. 4Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.” 5Hata ndugu zake pia hawakumwamini. 6Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari. 7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu. 8Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.” 9Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya. 10Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri. 11Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?” 12Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.” 13Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Germano, Patriarki wa Konstantinopoli (740)
- Kutangazwa mtakatifu kwa Mfiadini wa Kikasisi Hermogeni, Patriarki wa Moscow na Urusi yote, mtenda miujiza (1913)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro, padri (1937)
- Mtakatifu Mtawa Dionisio wa Radonezh (1633)
- Kupatikana kwa mara ya pili kwa masalia ya Mwenye Haki Simeoni wa Verkhoturye (1992)
- Maaskofu Watakatifu Sabino, Askofu Mkuu wa Kipro (karne ya 5), na maaskofu watakatifu wengine wa Kipro
- Askofu Mtakatifu Polibio, Askofu wa Rinokorura (karne ya 5)
- Mfiadini Yohana Mvlaki (1662) (Romania)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Mei katika kalenda ya kanisa ni 25 Mei katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki