Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 22 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Mei 2027

Jumamosi · Juma la 7 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 7 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Rita wa Kashia · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 103:13–18

13Kama vile baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Yahwe alivyo na huruma kwao wamchao. 14Maana anajua tulivyo umbwa; anajua kuwa tu mavumbi. 15Kama ilivyo kwa mwanadamu, siku zake ni kama majani; hustawi kama ua katika shamba. 16Upepo hulipiga, nalo hutoweka, na hakuna hata mmoja awezaye kuelezea mahali lilipokua. 17Lakini agano la uaminifu wa Yahwe uko kwa wale wamchao yeye milele hata milele. Haki yake ni endelevu kwa uzao wao. 18Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maagizo yake.

Injili

Mk 10:13–16

13Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. 14Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. 15Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. 16Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki