Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 21 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Mei 2027

Ijumaa · Juma la 7 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 7 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Kristofa Magallanes, padre, na wenzake, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 119:12, 16, 18, 27, 34–35

12Umetukuka, Yahwe; unifundishe amri zako. 16Ninafurahia katika amri zako; sitalisahau neno lako. 18Ufungue macho yangu ili niweze kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. 27Unifahamishe njia ya maagizo yako, ili niweze kutafakari juu ya mafundisho yako ya ajabu. 34Unipe uelewa, nami nitazishika sheria zako; nitazitii kwa moyo wangu wote. 35Uniongoze katika njia ya amri zako, maana ninafurahi kuenenda katika hizo.

Injili

Mk 10:1–12

1Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya. 2Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?” 3Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuru nini?” 4Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke.” 5“Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia. 6“Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.' 7Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, 8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” 10Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili. 11Akawaambia, “Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake. 12Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 21 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki