Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 23 Mei
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Mei 2027
Jumapili · Juma la 8 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Utatu Mtakatifu
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
32Kwa ajili ya kuuliza sasa kuhusu siku zilizopita ambazo zilikuwa mbele yenu: tangu siku ile ambayo Mungu alimuumba mtu katika nchi, kutoka pande moja ya mbingu hadi nyingine, uliza kama kumekuwepo chochote kama hiki kikubwa, au chochote kama hicho imewahi kusikiwa? 33Ilishawahi kutokea watu kusikia sauti ya Mungu kuongea katikati ya moto, kama mlivyosikia, na kuishi? 34Au Mungu ameshawahi kujaribu kwenda na kujichukulia kwa ajili yake taifa kutoka miongoni mwa taifa, kwa majaribu, ishara na maajabu na kwa vita, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoshwa, na magaidi wakuu, vile vyovyote ambavyo Yahwe Mungu wenu alifanya kwa ajili yenu Misri mbele ya macho yenu? 39Tambua hivi leo, weka kwenye moyo wako, Yahwe ni Mungu juu ya mbingu na chini ya dunia, hakuna mwingine yeyote. 40Mtazishika sheria zake na amri zake ambazo nawaamuru leo, ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu na watoto wenu baada yenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu amewapa milele.”
Wimbo wa katikati
4Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki. 5Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe. 6Kwa neno la Yahwe mbingu ziliumbwa, na nyota zote ziliumbwa kwa pumzi ya mdomo wake. 9Kwa maana yeye alisema, na ikafanyika; aliamuru, na ikasimama mahali pake. 18Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu 19kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa. 20Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. 22Yahwe, agano lako takatifu, liwe pamoja nasi tuwekapo tumaini letu katika wewe.
Somo la pili
14Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu. 15Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!” 16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu. 17Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.
Injili
16Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza. 17Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka. 18Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni. 19Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu. 20Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki