Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 20 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Mei 2027

Alhamisi · Juma la 7 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 7 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Bernardino wa Siena, padre · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 1:1–4, 6

1Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha. 2Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku. 3Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa. 4Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 6Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.

Injili

Mk 9:41–50

41Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake. 42Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini. 43Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto “usiozimika”. 45Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili. 47Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu. 48Mahali palipo na funza wasiokufa, na moto usiozimika. 49Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto. 50Chumvi ni nzuri, kama chumvi ikipoteza ladha yake, utaifanyaje iwe na ladha yake tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe, na muwe na amani kwa kila mmoja.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 20 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki