Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 20 Mei
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Mei (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Mei 2027
Alhamisi · Wiki ya 3 ya Pasaka · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Kumbukumbu ya kutokea kwa Msalaba wa Bwana angani juu ya Yerusalemu (351)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
26Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Njia hii iko katika jangwa). 27Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu. 28Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo. 30“Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?” 31Muethiopia akasema, “nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye. 32Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake: 33Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi.” 34Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine”?. 35Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu. 36Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?, 37maneno haya, “Hivyo Muethiopia akajibu “naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,” hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame. 38Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza. 39Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia.
Injili
40Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 41Kisha wayahudi wakamnung'unikia kumhusu yeye kwa sababu alisema, “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42Wakasema, “Huyu siyo Yesu mwana wa Yusuph, ambaye baba yake na mama yake tunamfahamu? Imekuwaje sasa anasema, 'Nimeshuka kutoka mbinguni'?” 43Yesu akajibu, akawambia, “Msinung'unikiane miongoni mwenu wenyewe. 44Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Akakio, akida (303)
- Mtakatifu Mtawa Nilo wa Sora (1508)
- Watakatifu Watawa Yohana wa Zedazeni na wanafunzi wake: Abibo, Askofu wa Nekresi, Antoni wa Martkopi, Daudi wa Gareja, Zenoni wa Ikalto, Thadayo wa Stepantsminda, Ise (Yese), Askofu wa Tsilkani, Yusufu, Askofu wa Alaverdi, Isidori wa Samtavisi, Mikaeli wa Ulumbo, Piro wa Breti, Stefano wa Khirsa na Shio wa Mgvime (karne ya 6) (Georgia)
- Kupatikana kwa masalia ya Nilo, anayetoa manemane, wa Athos (1815)
- Ikoni za Mama wa Mungu za Liubech (karne ya 11) na za Zhyrovichy (1470)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Mei katika kalenda ya kanisa ni 20 Mei katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki