Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 18 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Mei 2027

Jumanne · Juma la 7 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 7 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Yohane I, papa na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 37:3–4, 18–19, 27–28, 39–40

3Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani. 4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako. 18Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele. 19Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha. 27Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele. 28Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli. 39Wokovu wa haki unatoka kwa Yahwe; yeye huwalinda wao nyakati za shida. 40Yahwe huwasaidia na kuwaokoa. Yeye huwaokoa dhidi ya watu waovu na kuwanusuru wao kwa sababu wao wamemkimbilia yeye kwa ajili ya usalama.

Injili

Mk 9:30–37

30Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo, 31kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, “Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.” 32Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza. 33Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”? 34Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi. 35Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.” 36Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema, 37“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 18 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki