Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 20 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Aprili 2027
Jumanne · Juma la 4 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 4 la Pasaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
19Basi waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali, hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia. Waliwaambia ujumbe kuhusu Yesu peke yake kwa wayahudi na si kwa mwingine awaye yote. 20Lakini baadhi yao ni watu kutoka Kipro na Krene, walikuja Antiokia na kusema na wayunani na kumhubiri Bwana Yesu. 21Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na watu wengi waliamini na kumgeukia Bwana. 22Habari zao zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalem: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia. 23Alipokuja na kuona karama ya Mungu alifurahi; na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika mioyo yao. 24Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana. 25Baadaye Barnaba alienda Tarso kumwona Sauli. 26Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; 2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah 4Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'” 5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. 6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah 7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”
Injili
22Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu. 23Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani. 24Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi. 25Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu. 26Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu. 27Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi. 28Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu. 29Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba. 30Mimi na Baba tu mmoja.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki