Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 19 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 19 Aprili 2027
Jumatatu · Juma la 4 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 4 la Pasaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Mitume na ndugu wale waliokuwa huko Yudea walisikia kuwa wamataifa wamelipokea neno la Mungu. 2Petro alipokuja huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa, Wakisema, 3“Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!” 4Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema, 5“Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu. 6Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani. 7Kisha nikasikia sauti ikisema nami, “Amka, Petro, chinja naj ule!” 8Nikasema, “Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu” 9Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi, 10Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena. 11Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu. 12Roho akaniambia kwenda nao, na nisitofautiane nao. Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu mmoja. 13Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, “Nitume Yafa nikamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro. 14Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote.” 15Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni. 16Nakumbuka maneno ya Bwana, alivyosema, “Yohana alibatiza kwa maji; lakini mtabatizwa katika Roho mtakatifu.” 17Pia kama Mungu ametoa zawadi kama alizotupa sisi tulipoamini katika Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani, kwamba naweza kumpinga Mungu? 18Waliposikia mambo haya, hawakurudisha, bali walimsifu Mungu na kusema, “Mungu ametoa toba kwa ajili ya wa mataifa pia”
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah Kama ayala ayatamanivyo maji ya mto. ndivyo hivyo ninakiu yako, Mungu. 2Ninakiu yako Mungu, Mungu uliye hai, ni lini nitaonekana mbele zako? 43:3Oh, tuma nuru yako na kweli yako ziniongoze. Ziniletee mlima wako mtakatifu na makao yako. 4Kisha nitakwenda madhabahuni mwa Mungu, kwa Mungu wangu aliye furaha yangu kuu. Nami nitakusifu wewe kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu.
Injili
1Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi. 2Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje. 4Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake. 5Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.” 6Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao. 7Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo. 8Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza. 9Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho. 10Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki