Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 20 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Aprili (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Aprili 2027
Jumanne · Wiki ya 6 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Georgi Mwungamaji, Mitropoliti wa Mitilene (baada ya 820)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
6Asema hivi, ''Ni kitu kidogo sana kwa wewe kuwa mtumishi wangu ili kuanzisha ukoo wa Yakobo, na kuwarejesha wanaoishi Israeli. Nitakufanya wewe kuwa mwanga kwa Wayunani, ili uwe wokovu wangu katika mipaka ya nchi. 7Yahwe asema hivi, Mkombozi wa Israeli, Mtatakatifu wao, kwa yeye ambae maisha yake yamedharauliwa, kuchukiwa na mataifa, na mtumwa wa viongozi, ''Mfalme atakuona wewe na nyanyuka, na wakuu watakuona wewe na inama chini, kwa sababu ya Yahwe ambae ni mwaminifu, hata mtakatifu wa Israeli, aliyewachagua ninyi.'' 8Yahwe asema hivi, ''Kwa mda huu nimeamua kuwaonyesha neema yangu na nitawajibu ninyi, na siku ya wokovu nitawasaidi ninyi; Nitakulinda wewe; na nitawapa kama agano kwa watu, kuitengeneza tena nchi, kuwarihtisha urithi uliokuwa na ukiwa. 9Utasema kwa wafungwa, 'Tokeni nje; kwa wale mlio katika giza gerezani, 'Jionyeshe mwenyewe. 'Watachunga pembeni ya barabara, na juu ya miteremko ya wazi yatakuwa malisho yake. 10Hawatasikia njaa wala kiu; wala joto au jua halitawaunguza, kwa yeye mwenye huruma juu yao atawaongoza wao; atawaongoza wao kwenye mikondo ya maji.
Sala ya Jioni: somo
3Kisha Yahwe akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na ya ndugu zako, nami nitakuwa nawe.” 4Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwandani katika kundi lake la kondoo 5naye akawambia, “Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa nami. 6Nanyi mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu. 7Baba yenu amenidanganya na amebadilisha ujira wangu mara kumi, lakini Mungu hakumruhusu kunidhuru. 8Ikiwa alisema, 'Wanyama wenye mabaka watakuwa ujira wako,' ndipo kondoo wote walipozaa watoto wenye mabaka. Na aliposema, wenye milia watakuwa ujira wako,' ndipo kundi lote lilipozaa watoto wenye milia. 9Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi. 10Wakati fulani wa majira ya kupandana, niliona katika ndoto mabeberu yaliyowapanda kundi. Mabeberu yalikuwa ya milia, mabaka na madoa. 11Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.' 12Akasema, 'Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea. 13Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa. 14Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, “Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu? 15Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu. 16Mali zote ambazo sasa Mungu amemnyang'anya baba yetu ni zetu na watoto wetu. Sasa basi, lolote Mungu alilokuambia, fanya.
Sala ya Jioni: somo
3Kutenda haki na adili hukubaliwa zaidi na Yehova kuliko sadaka. 4Macho ya kiburi na moyo wa majivuno- taa ya waovu- ni dhambi. 5Mipango ya mwenye juhudi huelekea kwenye mafanikio tu, bali kila mtu anayetenda kwa haraka huelekea umasikini. 6Kujipatia utajiri kwa ulimi wa uongo ni mvuke unaopita upesi na mtego ambao unafisha. 7Vurugu ya waovu itawaburuta mbali, maana wanakataa kutenda haki. 8Njia ya mwenye hatia ni ukatiri, bali mwenye usafi hutenda yaliyo ya haki. 9Bora kuishi kwenye kona ya juu darini kuliko katika nyumba pamoja na mke mgonvi. 10Hamu ya mwovu ni uchu wa mabaya; jirani yake haoni ukarimu katika macho yake. 11Mwenye dhihaka anapoadhibiwa mjinga hupata busara, na mtu mwenye busara anapofundishwa, anaongeza maarifa. 12Atendaye haki huilinda nyumba ya mwovu; huwashusha waovu kwenye uharibifu. 13Anayeziba masikio yake kwenye kilio cha masikini, pia atalia, lakini hatajibiwa. 14Zawadi ya siri hutuliza hasira na zawadi ya kificho hutuliza ghadhabu kuu. 15Haki ikitendeka, huleta furaha kwa mwenye kutenda wema, lakini huleta hofu kubwa kwa watenda mabaya. 16Yule anayezurura kutoka kwenye njia ya ufahamu, atapumzika kwenye kusanyiko la wafu. 17Anayependa raha atakuwa masikini; anayependa divai na mafuta hawezi kuwa tajiri. 18Mtu mbaya ni fidia kwa yule atendaye haki, na mdanganyifu ni fidia kwa waaminifu. 19Bora kuishi jangwani kuliko kuishi pamoja na mwanamke ambaye huchochea sana ugomvi na malalamiko. 20Hazina yenye thamani na mafuta vipo nyumbani kwa mwenye busara, bali mtu mpumbavu huviharibu. 21Mtu atendaye haki na mwema -huyu mtu hupata uzima, haki na heshima.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Arkadio, padri (1933)
- Mtawa Mfiadini Eudokia (1939)
- Mtakatifu Mtawa Danieli wa Pereslavl (1540)
- Mfiadini Kaliopio (304)
- Wafiadini Rufino, shemasi, Akilina na pamoja nao askari 200 (karibu 310)
- Mtakatifu Mtawa Serapioni, mtawa wa Misri (karne ya 5)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Aprili katika kalenda ya kanisa ni 20 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki