Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 21 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Aprili 2027

Jumatano · Juma la 4 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 4 la Pasaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Anselmi wa Canterbury, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 12:24–13:5

24Lakini neno la Mungu likakua na kusambaa. 25Baada ya Barnaba na Sauli kukamilisha huduma yao wakatoka pale wakarejea Yerusalemu, wakamchukua na Yohana ambaye jina la kuzaliwa ni Marko. 13:1Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni(ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli. 2Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.” 3Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende. 4Kwa hiyo Barnabas na Sauli walimtii Roho Mtakatifu na walitelemka kuelekea Seleukia; Kutoka huko walisafiri baharini kuelekea kisiwa cha Kipro. 5Walipokuwa katika mji wa Salami, walilitangaza neno la Mungu katika Masinagogi ya Wayahudi. Pia walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.

Wimbo wa katikati

Zab 67:1–2, 4–5, 7

1Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo. Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah 2ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. 4Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 5Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 7Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.

Injili

Yn 12:44–50

44Yesu akapaza sauti na kusema, “Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi, 45naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma. 46Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47Ikiwa mtu yeyote atayasikia maneno yangu lakini asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu. 48Yeye anikataye mimi na asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Maana mimi sikunena kwa nafsi yangu tu. Bali ni Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi - kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 21 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki