Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 16 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Aprili 2027

Ijumaa · Juma la 3 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 3 la Pasaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 9:1–20

1Lakini Sauli, aliendelea kusema vitisho hata vya kifo kwa wanafunzi wa Bwana, alikwenda kwa kuhani mkuu 2na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,' 4naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia,”Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?” 5Sauli akajibu, U nani wewe Bwana? Bwana akasema, “ Mimi ndiye Yesu unayeniudhi; 6Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda 7Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakatulia kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu. 8Sauli akainuka katika nchi na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi. 10Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania, Bwana alisema naye katika maono, “Anania.” Na akasema, “Tazama, nipo hapa, Bwana. 11“Bwana akamwambia, “Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba; 12na alimwona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili kwamba apate kuona. 13Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, kwa kiasi gani alivyowatendea mabaya watakatifu wa huko Yerusalemu; 14Hapa ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja anayeliitia jina lako. 15Lakini Bwana akamwambia, “Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, alichukue jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Israeli. 16Maana nitawaonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu”. 17Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu. 18Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu. 19Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi. 20Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Wimbo wa katikati

Zab 117:1–2

1Msifuni Yahwe, enyi mataifa yote; enyi watu mhimidini yeye. 2Kwa kuwa uaminifu wa agano lake ni mkuu kwetu, na uaminifu wa Yahwe wadumu milele. Msifuni Yahwe.

Injili

Yn 6:52–59

52Wayahudi wakakasirika wenyewe kwa wenyewe na wakaanza kubishana wakisema, “Mtu huyu anawezaje kutupa mwili wake tuule?” 53Kisha Yesu akawambia, “Amini, amini, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamta kuwa na uzima ndani yenu. 54Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake. 57Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, na yeye pia ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele. 59Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.

Watakatifu wa 16 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki