Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 17 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Aprili 2027
Jumamosi · Juma la 3 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 3 la Pasaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
31Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na kutembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi. 32Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, akawateremkia waumini waishio katika mji wa Lida. 33Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, mtu huyo amekuwa kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. 34Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo akuponye; Amka na ujitandikia kitanda chako,” Mara akaamka. 35Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni walipomuona mtu huyo, walimgeukia Bwana. 36Palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha, ambalo lilitafsiriwa kama “Dorcas” Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya rehema aliyoyafanya kwa maskini. 37Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza.. 38Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, “Njoo kwetu bila kuchelewa”. 39Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha koti na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati akiwa pamoja nao. 40Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, “Tabitha, amka”. Akafungua macho yake na alipomwona Petro akakaa chini. 41Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita waamini na wajane, akawakabidhi kwao akiwa hai 42Jambo hili likajulikana Yafa yote, na watu wengi wakamwamini Bwana.
Wimbo wa katikati
12Nimlipeje Yahwe kwa wema wake wote kwangu? 13Nitakiinua kikombe cha wokovu, na kuliitia jina la Yahwe. 14Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote. 15Mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pa Mungu. 16Ee Yahwe, hakika, mimi ni mtumishi wako; mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umefungua vifungo vyangu. 17Nitakutolea dhabihu ya shukrani na nitaliitia jina la Yahwe.
Injili
60Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?” 61Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza? 62Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla? 63Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima. 64Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti. 65Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba.” 66Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena. 67Yesu akawambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?” 68Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele, 69na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki