Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 15 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 15 Aprili 2027
Alhamisi · Juma la 3 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 3 la Pasaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
26Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Njia hii iko katika jangwa). 27Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu. 28Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo. 30“Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?” 31Muethiopia akasema, “nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye. 32Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake: 33Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi.” 34Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine”?. 35Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu. 36Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?, 37maneno haya, “Hivyo Muethiopia akajibu “naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,” hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame. 38Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza. 39Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia. 40Lakini Philipo akatokea Azoto. Alipita katika mkoa ule na kuhubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
Wimbo wa katikati
8Mtukuzeni Mungu, enyi watu wa mataifa yote, sauti ya sifa zake isikike. 9Yeye atuwekaye hai, naye hairuhusu miguu yetu iteleze. 16Njoni, msikie, ninyi nyote mnao mwabudu Mungu, nami nitatangaza yale yeye aliyoitendea roho yangu. 17Nilimlilia kwa kinywa changu, naye alipendezwa na ulimi wangu. 20Atukuzwe Mungu, ambaye hakuyakataa maombi yangu wala kuweka uaminifu wa agano lake mbali nami.
Injili
44Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. 45Kwa kuwa imeandikwa katika manabii, 'Watafundishwa na Mungu.' Kila aliyesikia na amejifunza kutoka kwa Baba, huja kwangu. 46Sio kwamba kuna mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu- amemwona Baba. 47Amini, amini yeye aaminiye anao uzima wa milele. 48Mimi ni mkate wa uzima. 49mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa. 50Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife. 51Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki