Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 14 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Aprili 2027

Jumatano · Juma la 3 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 3 la Pasaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 8:1–8

1Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. siku hiyo ndipo alipoanza kuwatesa kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote waliotawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume. 2Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake. 3Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwaburuza nje wanawake na waume, na kuwatupia gerezani. 4waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walilihubiri neno. 5Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko. 6Baada ya makutano kusikia na kuona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichosema. 7Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa, na wengi waliopooza na viwete waliponywa. 8Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.

Wimbo wa katikati

Zab 66:1–7

1Kwa kiongozi wa muziki. Wimbo, Zaburi. Mpigieni Mungu kelele za shangwe, nchi yote; 2Imbeni utukufu wa jina lake; mzitukuze sifa zake. 3Mwambieni Mugu, “Matendo yako yanatisha kama nini! Kwa ukuu wa nguvu zako maadui zako watajisalimisha kwako. 4Nchi yote watakuabudu wewe na watakuimbia wewe; wataliimbia jina lako.” Selah 5Njoni na mtazame kazi za Mungu; yeye anatisha katika matendo yake awatendeayo wanadamu. 6Aligeuza bahari kuwa nchi kavu; wao walitembea kwa mguu juu ya mto; huko tulishangilia katika yeye. 7Yeye anatawala milele kwa nguvu zake; macho yake yanachunguza mataifa; waasi wasijivune. Selah

Injili

Yn 6:35–40

35Yesu akawambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima, yeye ajaye kwangu hatapata njaa na yeye aniaminiye hatahisi kiu kamwe.” 36Ingawa niliwaambia kwamba, mmeniona, na bado hamuamini. 37Wote ambao Baba anaonipa watakuja kwangu, na yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kabisa. 38Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni, sio kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma. 39Na haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali nitawafufua siku ya mwisho. 40Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Watakatifu wa 14 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki