Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 1 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 19 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 1 Aprili 2027
Alhamisi · Wiki ya 3 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Krisantho na Daria, na pamoja nao Wafiadini Klaudio, jemadari, Hilaria, mke wake, Yasoni na Mauro, wana wao, Diodoro, padri, na Mariano, shemasi (283)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
10Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka. 11Siku hiyo, Bwana ataunyoosha mkono wake tena kuokoa mabaki ya watu wake yaliyosalia huko Asiria, Misri, Pathrosi, Kushi, Shinari, Hamathi, na kisiwa cha bahari. 12Ataweka bendera kwa kwa mataifa na atakusanya Waisrel waliotupwa na watu wa Juuda waliotawanyika kitika pembe nne za dunia. 13Ataujeuza wivu wa Efraimu, na ukatili wa Yuda utakomeshwa. Efraimu atamuonea wivu Yuda, Yuda hatakuwa adui wa Efraimu tena. 14Badala yake, watashuka chini kwenye mlima wa Wafilisti upande wa magharibi, na pamoja watateka watu mashariki. Watavamia Edomu na Moabu, na watu wa Amoni watawatii wao. 15Yahwe atauharibu kabisa ghuba ya bahari ya Misri. Kwa mawimbi makali ambayo yanavuma juu ya mtoto Efurate na itagawanyika katika mifereji saba, hivyo unaweza ukapita juu kwa viatu. 16Kutakuwa na njia kuu kwa ajili ya mabaki ya watu kurudi kutoka Asiria, maana kuna Waisraeli wanaokuja kutoka nchi ya Misri. 12:1Siku hiyo utasema, ''Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi, 2Ona Bwana ni wokovu wangu; nitamwamini na sitakuwa na hofu, kwa Yahwe, ndio, Yahwe ni nguvu yangu na wimbo wangu. Amekuwa wokovu wangu.''
Sala ya Jioni: somo
11Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka. 12Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku. 13Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina. 14Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa. 15Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina. 16Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango. 17Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi. 18Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa. 20Maji yakaongezeka dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima. 21Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu. 22Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa. 23Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa mchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia. 24Maji haya kuzama chini ya nchi kwa muda wa siku miamoja na hamsini. 8:1Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini. 2Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha. 3Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi. na mwisho wa siku miamoja na hamsini maji yakawa yamezama chini.
Sala ya Jioni: somo
1Mithali za Sulemani. Mwana mwenye hekima humfurahisha baba yake lakini mwana mpumbavu huleta majonzi kwa mama yake. 2Hazina zilizolimbikizwa kwa uovu hakosa thamani, bali kwa kutenda haki hujilinda mbali na kifo. 3Yehova hawaachi wale watendao haki wapate njaa, bali hamu ya waovu huizuia. 4Mkono mlegevu humfanya mtu awe masikini, bali mkono wa mtu mwenye bidii hupata utajiri. 5Mwana mwenye busara hukusanya mazao wakati wa kiangazi, bali ni aibu kwake alalaye wakati wa mavuno. 6Zawadi kutoka kwa Mungu zipo juu ya kichwa cha wale watendao haki; bali kinywa cha uovu hufunikwa kwa jeuri. 7Mtu atendaye haki anatufurahisha tunapomkumbuka, bali jina la mwovu litaoza. 8Wale wenye akili hukubali maagiza, bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataangamia. 9Yeye anayetembea katika uadilifu hutembea katika usalama, bali yule anayepotosha njia zake, ataonekana. 10Yeye ambaye hukonyeza kwa jicho lake huleta majonzi, bali mpumbavu mwenye maneno mengi atatupwa chini. 11Kinywa cha mwenye kutenda haki ni kama chemchemi ya maji ya uzima, bali kinywa cha uovu hufunikwa kwa jeuri. 12Chuki huchochea mafarakano, bali upendo hufunika juu ya makwazo yote. 13Hekima inapatikana kwenye kinywa cha mtu mwenye ufahamu, bali fimbo ni kwa ajili ya mgongo wa yule asiye na akili. 14Watu wenye hekima hutunza maarifa, bali kinywa cha mpumbavu huleta uharibifu karibu. 15Mali ya mtu tajiri ni mji wake mwenye ngome; ufukara wa masikini ni uharibifu wao. 16Mshahara wa watenda haki huelekea kwenye uzima; manufaa ya waovu huelekea dhambini. 17Kuna njia kwenda kwenye uzima kwa yule anayefuata maongozo, bali anayekataa maonyo hupotea. 18Yeye afichaye chuki anamidomo ya uongo, na yeye anayesambaza kashfa ni mpumbavu. 19Katika maneno mengi, hapakosi uhalifu, bali aliyemwangalifu katika usemi wake ni mwenye busara. 20Ulimi wa yule atendaye haki ni fedha safi; kuna thamani ndogo katika moyo wa mbaya. 21Midomo ya yule atendaye haki huwastawisha wengi, bali wapumbavu hufa kwa sababu ya kukosa akili. 22Zawadi njema za Yehova huleta utajiri na haweki maumivu ndani yake.
Watakatifu wa siku
- Mwenye Haki Sofia, binti wa mfalme wa Slutsk (1612)
- Mtakatifu Yohana Mwungamaji (1932)
- Mtawa Mfiadini Matrona (1938)
- Mfiadini Pankario (karibu 302)
- Mtakatifu Mtawa Vasa wa Mapango ya Pskov († karibu 1473)
- Mtakatifu Mtawa Inokenti wa Komel, wa Vologda (1511-1522)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Smolensk iitwayo “Huruma” (1103)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 19 Machi katika kalenda ya kanisa ni 1 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki