Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 31 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 18 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 31 Machi 2027

Jumatano · Wiki ya 3 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 2

Sikukuu na watakatifu

Askofu Mtakatifu Kirilo, Askofu Mkuu wa Yerusalemu (386)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 10:12–20

12Pindi ambapo Bwana alipoimaliza kazi kwenye mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu maneno ya moyo wenye kiburi ya mfalme wa Asiria na majivuno yake. 13Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake. 14Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.'' 15Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je litajisifia lenyewe zaidi ya yule anaelitumia kukatia? Au fimbo imuinuae yeye ambaye si mti. 16Hivyo basi Yahwe wa majeshi atatuma wadhaifu miongoni mwa wasomi wa kijeshi; na chini ya utukufu na kuteketea kama kuteketea kwa moto. 17Mwanga wa Isreli utakuwa moto, na Mtakatifu wake atakuwa ni moto unaoteketeza na kula mbigiri siku moja. 18Yahwe atauteketeza utukufu wa msitu wake na shamba lake linalostawi, vyote nafsi na mwili; itakuwa kama vile mgonjwa apotezae maisha yake. 19Mabaka ya miti ya misitu itakuwa michache sana, ambayo mtoto anaweza kuyahesabu. 20Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 7:6–9

6Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia sita wakati gharika ilipokuja juu ya nchi. 7Nuhu, watoto wake wa kiume, mke wake, na wake za watoto wake waliingia katika safina pamoja kwa sababu ya maji ya gharika. 8Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi, 9wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu.

Sala ya Jioni: somo

Mit 9:12–18

12Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako. 13Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote. 14Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji. 15Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao. 16Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!” anawaambia wale wasio na akili. “ 17Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza.” 18Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 31 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 18 Machi katika kalenda ya kanisa ni 31 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki