Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 31 Machi
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 31 Machi 2027
Jumatano · Oktava ya Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano katika Oktava ya Pasaka
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Sasa Peter na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa. 2Mtu fulani, kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu uitwao mzuri, ili aweze kuomba sadaka kutoka kwa watu waliokuwa wakielekea hekaluni. 3Alipowaona Petro na Yohana wanakaribia kuingia hekaluni, aliomba sadaka. 4Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, alisema,”tutazame sisi.” 5Kiwete akawatazama, akitazamia kupokea kitu fulani kutoka kwao. 6Lakini Petro akasema, “fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitatoa kwako. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea.” 7Petro akamchukua kwa mkono wake wa kulia, na akamwinua juu: mara moja miguu yake na vifundo vya mifupa yake vikapata nguvu. 8Akiruka juu, mtu kiwete alisimama na akaanza kutembea; akaingia hekaluni pamoja na Petro na Yohana, akitembea, akiruka, na kumsifu Mungu. 9Watu wote walimwona akitembea na akimsifu Mungu. 10Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu ambaye alikuwa akikaa akiomba sadaka kwenye mlango mzuri wa hekalu; walijawa na mshangao na kustaajabu kwa sababu ya kile kilichotokea kwake.
Wimbo wa katikati
1Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa. 2Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau. 3Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi. 4Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. 6miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake. 7Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote. 8Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu. 9Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka.
Injili
13Na tazama, wawili miongoni mwao walikuwa wakienda siku hiyo hiyo katika kijiji kimoja kiitwacho Emmau, ambacho kilikuwa maili sitini kutoka Yerusalemu. 14Wakajadiliana wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotokea. 15Ikatokea kwamba, wakati walipokuwa wakijadiliana na kuulizana maswali, Yesu akasogea karibu akaambatana nao. 16Lakini macho yao yalizuiliwa katika kumtambua yeye. 17Yesu akawaambia, “Nini ambacho ninyi wawili mnakiongelea wakati mnatembea?” Wakasimama pale wakionekana na huzuni. 18Mmoja wao, jina lake Cleopa, akamjibu, “Je wewe ni mtu pekee hapa Yerusalemu ambaye hajui mambo yaliyotokea huko siku hizi?” 19Yesu akawaambia, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo kuhusu Yesu Mnazareti, ambaye alikuwa nabii, muweza katika matendo na maneno mbele za Mungu na watu wote. 20Na kwa jinsi ambayo wakuu wa makuhani na viongozi wetu walivyomtoa kuhukumiwa kifo na kumsulubisha. 21Lakini tulitumaini kwamba yeye ndiye atakaye waweka huru Israeli. Ndiyo, mbali na haya yote, sasa ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22Lakini pia, baadhi ya wanawake kutoka katika kundi letu walitushangaza, baada ya kuwapo kaburini asubuhi na mapema. 23Walipoukosa mwili wake, wakaja, wakisema kwamba waliona pia maono ya malaika waliosema kwamba yu hai. 24Baadhi ya wanaume ambao walikuwa pamoja nasi walienda kaburini, na kukuta ni kama vile wanawake walivyosema. Lakini hawakumuona yeye.” 25Yesu akawaambia, “Ninyi watu wajinga na wenye mioyo mizito ya kuamini yote ambayo manabii wamesema! 26Je haikuwa lazima Yesu kuteseka kwa mambo haya, na kuingia katika utukufu wake?” 27Kisha kuanzia kutoka kwa Musa na manabii wote, Yesu akawatafsiria mambo yanayomuhusu yeye katika maandiko yote. 28Walipokaribia kile kijiji, huko walikokuwa wakienda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea mbele. 29Lakini walimlazimisha, wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana inaelekea jioni na siku ni kama imeisha.” Hivyo Yesu akaingia kwenda kukaa nao. 30Ilitokea kwamba, wakati amekaa nao kula, alichukua mkate, akaubariki, na kuuvunja, akawapa. 31Kisha macho yao yakafunguliwa, wakamjua, na akatoweka ghafla mbele ya macho yao. 32Wakasemezana wao kwa wao, “Hivi mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, wakati alipoongea nasi njiani, wakati alipotufungulia maandiko?” 33Wakanyanyuka saa hiyo hiyo, na kurudi Yerusalemu. Wakawakuta wale kumi na mmoja wamekusanyika pamoja, na wale waliokuwa pamoja nao, 34wakisema, “Bwana amefufuka kwelikweli, na amemtokea Simoni.” 35Hivyo wakawaambia mambo yaliyotokea njiani, na namna Yesu alivyodhihirishwa kwao katika kuumega mkate.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki