Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 22 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Machi 2027

Jumatatu · Wiki ya 2 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 1

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini 40 waliouawa katika ziwa la Sebastia: Kirioni, Kandido, Domno, Hesikio, Iraklio, Smaragdo, Eunoiko, Valente, Viviani, Klaudio, Prisko, Theodulo, Eutikio, Yohana, Ksanthio, Iliani, Sisinio, Angio, Aetio, Flavio, Akakio, Ekdikio, Lisimako, Aleksanda, Ilio, Gorgonio, Theofilo, Dometiani, Gayo, Leontio, Athanasio, Kirilo, Sakerdoni, Nikolao, Valerio, Filoktimoni, Severiani, Khudioni, Melitoni na Aglaio († karibu 320)

Kwaresima Kuu

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Sala ya Alfajiri: Injili (Mashahidi)

Lk 21:12–19

12Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu. 13Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu. 14Kwahiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema, 15kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana. 16Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu. 17Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu. 18Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea. 19Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.

Saa ya 6

Isa 4:2–5:7

2Na siku hiyo tawi zuri la Yahwe na utukufu, na matunda yatakuwa na ladha nzuri na kupendeza kwa wale wanaoishi Israeli. 3Itatokea kwa yule aliyeachwa Sayuni na wale waliobakia Yerusalemu wataitwa watakatifu, yeyeto aliyeandikwa chini anaishi Yerusalemu. 4Hii itatokea pale ambapo Bwana atasafisha uchafu wa mabinti wa Sayuni, na atasafisha madoa ya damu kutoka kati ya Yerusalemu, kwa namna ya roho ya hukumu na roho ya kuungua na moto. 5Tena juu ya mlima wote wa Sayuni na mahali pakuksanyikia, Yahwe atafanya wingu na moshi kwa wakati wa mchana na moto unaong'a wakati wa usiku; na itakuwa dari juu ya utukufu wote. 6kutakuwa na kivuli kwenye makazi wakati mchana kuzuia jua, na kimbilio na mfuniko kutoka kwenye mawimbi na mvua. 5:1Acha niimbe kwa mpendwa wangu mzuri, wimbo wa mpendwa wangu kuhusu shamba la mzabibu. Mpendwa wangu ana shamba kwenye mlima wenye rutuba. 2Analilima, anaondoa mawe, na anaotesha aina ya mizabibu iliyo bora. Na hujenga mnara katikati ya shamba akichimba shinkizo ndani yake. Anasubiria mzabibu uzae matunda lakini unazaa zabibu mwitu. 3Kwa hiyo sasa, wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda, toa hukumu kati yangu na shamba la mzabibu. 4Je ni kitu gani cha ziada unaweza ukakifanya kwenye shamba langu la mizabibu, ambacho sijakifanya? ninapotamzamia izae matunda, kwa nini inazaa matunda mwitu? 5Sasa nitawambia kitu nitakacho kifanya kwenye shamba langu la mzabibu: nitaondoa uzio, nitaligeuza kuwa malisho, Nitavunja ukuta wake chini. Na itakanyagwa chini. 6Nami nitaliharibu wala halitapaliliwa wala kuilmwa, bali litatoa mbigiri na miba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshee mvua juu yake. 7Maana shamba la mzabibu la Yahwe Bwana wa majeshi ni nyumba ya Israeli, na mtu wa Yuda ndio mazao yake ya kupendeza; anaisubiria haki lakini badala ya yaki kuna mauwaji; maana haki, lakini badala yake ni kelele zikihitaji msaada.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 3:21–4:7

21Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha. 22Yahwe Mungu akasema, “ sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele.” 23Kwa hiyo Yahwe Mungu akamuondoa kutoka kwenye bustani ya Edeni, kwenda kulima ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa. 24Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima. 4:1Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, “ nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe.” 2Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo. 3Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe. 4Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake, 5lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana. 6Yahwe akamwambia Kaini, “ kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana? 7Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde.

Sala ya Jioni: somo

Mit 3:34–4:22

34Yeye huwadhihaki wenye dhihaka, bali huwapa hisani watu wanyenyekevu. 35Watu wenye busara huirithi heshima, bali wapumbavu huinuliwa kwa fedheha yao wenyewe. 4:1Wanangu, sikilizeni, fundisho la baba, na zingatieni ili mjue maana ya ufahamu. 2Mimi ninawapa mafundisho mazuri; msiyaache mafundisho yangu. 3Mimi nilikuwa mwana kwa baba yangu, mpole na mtoto pekee kwa mama yangu, 4baba alinifundisha akiniambia, “Moyo wako uzingatie sana maneno yangu; shika amri zangu nawe uishi. 5Jipatie hekima na ufahamu; usisahau na kuyakataa maneno ya kinywa changu; 6usiiache hekima nayo itakulinda; ipenda nayo itakuhifadhi salama. 7Hekima ni kitu cha muhimu sana, hivyo jipatie hekima na tumia namna zote kuweza kupata ufahamu. 8Tunza hekima nayo itakutukuza; ikumbatie nayo itakuheshimu. 9Hekima itaweka kilemba cha heshima juu ya kichwa chako; itakupa taji zuri. 10Mwanangu, sikiliza, na kuzingatia maneno yangu, nawe utapata miaka mingi ya maisha yako. 11Ninakuelekeza katika njia ya hekima, nimekuongoza katika mapito yaliyonyooka. 12Unapotembea, hakuna atakayesimama katika njia yako na kama ukikimbia hutajikwaa. 13Shika mwongozo wala usiuache, utakuongoza, maana ni uzima wako. 14Usifuate njia ya waovu wala usiende katika njia ya watendao uovu. 15Jiepushe nayo, usipite katika njia hiyo; geuka na upite njia nyingine. 16Maana hawawezi kulala mpaka wafanye ubaya na hupotewa na usingizi hadi wasababishe mtu kujikwaa. 17Maana wao hula mkate wa uovu na hunywa divai ya vurugu. 18Bali njia ya mwenye kutenda haki ni kama mwanga ung'aao, huangaza zaidi na zaidi hadi mchana inapowasili kwa ukamilifu. 19Njia ya waovu ni kama giza - hawajui ni kitu gani huwa wanajikwaa juu yake. 20Mwanangu, zingatia maneno yangu; sikiliza kauli zangu. 21Usiziache zikaondoka machoni pako; uzitunze katika moyo wako. 22Maana maneno yangu ni uzima kwa wenye kuyapata na afya katika mwili wao.

Sala ya Jioni: somo (Mashahidi)

Isa 43:9–14

9Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, 'kama ni kweli'. 10Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu. 11Mimi, Mimi Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu. 12Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, ''Mimi ni Mungu. 13Kuanzia leo na kuendelea mimi ndiye, na hakuna hata mmoja atakayewakomboa kwenye mkono wangu. Nitafanya, na nani awezae kunizuia?'' 14Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: ''Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli' kuwa wimbo wa maombolezo.

Sala ya Jioni: somo (Mashahidi)

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo (Mashahidi)

Haimo katika tafsiri hii

Waraka (Mashahidi)

Ebr 12:1–10

1Kwahiyo, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa la mashaidi, na tutupe kila kitu kinacho tulemea pamoja na dhambi ambayo inatuzingira kwa urahisi. Tupige mbio kwa saburi katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu. 2Tuyaelekeze macho yetu kwa Yesu, aliye mwanzilishi na mwenye kutimiliza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahmili msalaba, akiidharau aibu yake, na akakaa chini mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu. 3Maana mtafakarini yeye aliye stahimili maneno ya chuki kutoka kwa wenye dhambi, dhidi yake mwenyewe ili kwamba msije mkachoka au kuzimia mioyo yenu. 4Hamjataabika au kuteseka mkishindana na dhambi kiasi cha kuishiwa damu. 5Tena mmesahau kule kutiwa moyo ambako kunawaelekeza kama watoto wa kiume: “Mwanangu, usiyachukuwe kwa wepesi marudia ya Bwana, wala usikate tamaa unapo rekebishwa na yeye.” 6Kwa kuwa Bwana humrudi yeyote ambaye anampenda, na humwadhibu kila mwana ambaye humpokea. 7Stahimili majaribu kama kurudiwa. Mungu hushughulika nanyi kama anavyoshughulika na watoto, maana ni mtoto yupi ambaye baba yake hawezi kumrudi? 8Lakini kama hakuna kurudiwa, ambako sisi sote tunashiriki, basi ninyi ni haramu na si watoto wake. 9Zaidi ya yote, tulikuwa na baba zetu kidunia wa kuturudi, na tuliwaheshimu. Je haitupasi hata zaidi kumtii Baba wa kiroho na kuishi? 10Kwa hakika baba zetu walituadhibu kwa miaka michache kama ilivyoonekana sawa kwao, lakini Mungu hutuadhibu kwa faida yetu ili tushiriki utakatifu wake.

Injili (Mashahidi)

Mt 20:1–16

1Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu. 2Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu. 3Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko. 4Akawaambia, 'Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.' Hivyo wakaenda kufanya kazi. 5Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo. 6Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, 'kwanini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima? 7Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, 'Nanyi ninyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.' 8Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, 'Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.' 9Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari. 10Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu. 11Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba. 12Wakasema, 'Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.' 13Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, 'Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja? 14Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe. 15Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema? 16Hivyo wa mwisho atakuwa kwanza na wa kwanza wa mwisho''

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Machi katika kalenda ya kanisa ni 22 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki