Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 23 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Machi 2027
Jumanne · Wiki ya 2 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Kodrato na wale walio pamoja naye: Kiprian, Dionisio, Anekto, Paulo, Kreske, Dionisio (mwingine), Viktorino, Vikta, Nikeforo, Klaudio, Diodoro, Serapioni, Papio, Leonida, na Wafiadini Hariesa, Nunekia, Basilisa, Nike, Gali, Galina, Theodora na wengine wengi (250-258)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
7Maana shamba la mzabibu la Yahwe Bwana wa majeshi ni nyumba ya Israeli, na mtu wa Yuda ndio mazao yake ya kupendeza; anaisubiria haki lakini badala ya yaki kuna mauwaji; maana haki, lakini badala yake ni kelele zikihitaji msaada. 8Ole wao wanaoungana nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba, mpaka wanamaliza, na umebaki mwenyewe kwenye shamba! 9Yahwe wa majeshi ameniambia mimi, nyumba nyingi zitakuwa wazi, hata kubwa na zinazovutia, hakuna mwenyeji yeyote. 10Maana mashamba ya mizabibu la nira kumi lilitoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu. 11Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema kutafuta pombe kali, wale wanaokaa usiku wa manane mpaka pombe inawaka moto. 12Wanasherekea kwa kinubi, kinanda, kigoma, filimbi, na mvinyo, lakini hawazitambui kazi za Yahwe, wala hawaziangalii kazi za mikono yake. 13Kwa hiyo watu wangu wameenda kifungoni kwa kukosa uelewa; viongozi wao wakuheshimiwa wanashinda na njaa, na watu wao hana kitu cha kunjwa. 14Hivyo basi kuzimu kumeongeza ladha yake na imefungua kinywa chake kwa kiasi kikubwa; wasomi wao, viongozi wao, manabii na wenye furaha miongoni mwao, watashuka kuzimu. 15Mtu atalazimishwa kuinama chini, na watu watakuwa wayenyekevu; na macho yao ya kujivuna yatatupwa chini, 16Yahwe wa majeshi atainuliwa katika haki yake, na Mungu mtakatifu atajidhirisha kuwa mtakatifu kwa haki yake.
Sala ya Jioni: somo
8Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua). 9Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” 10Yahwe akasema, “umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini. 11Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako kutoka mikononi mwako. 12Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.” 13Kaini akamwambia Yahwe, “Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili. 14Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.” 15Yahwe akamwambia, “ikiwa mtuyeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba.” Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu awayeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.
Sala ya Jioni: somo
1Mwanangu, zingatia hekima yangu; sikiliza kwa makini ufahamu wangu, 2ili ujifunze busara na midomo yako iweze kuhifadhi maarifa. 3Maana midomo ya malaya hutiririsha asali na kinywa chake ni laini kuliko mafuta, 4lakini mwishoni anakuwa mchungu kama mnyoo, hukata kama upunga mkali. 5Miguu yake huelekea mauti; hatua zake huelekea njia yote ya kuzimu. 6Hafikirii njia ya uzima. Hatua za miguu yake hupotea, maana hajui anakwenda wapi. 7Sasa, wanangu, nisikilizeni; wala msiache kusikiliza maneno ya kinywa changu. 8Lindeni njia yenu mbali naye wala msiende karibu na mlango wa nyumba yake. 9Kwa njia hiyo hamtawapa wengine heshima yenu au miaka ya uzima wenu kwa mtu mkatiri; 10wageni usije kufanya karamu kwa utajiri wenu; kazi mliyoifanya haitaenda katika nyumba ya wageni. 11Mwishoni mwa maisha yenu mtajuta ambapo nyama na mwili wenu vitaangamia. 12Nanyi mtasema, “ Namna gani nilichukia fundisho na moyo wangu ulidharau sahihisho! 13Sikuweza kuwatii walimu wangu au kuwasikiliza walionielekeza. 14Nilikuwa nimeharibika kabisa katikati ya kusanyiko, miongoni mwa makutano ya watu.” 15Munywe maji kutoka kwenye birika lenu mwenyewe na munywe maji yanatiririka kutoka kwenye kisima chenu.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Demetrio, padri (1938)
- Wafiadini Kodrato wa Nikomedia, Satorino, Rufino na wengine (karne ya 3)
- Mtakatifu Mtawa Anastasia, mtukufu (567-568)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Machi katika kalenda ya kanisa ni 23 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki