Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 8 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 26 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 8 Februari 2027
Jumatatu · Wiki ya 37 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Watakatifu Watawa Ksenofoni, mke wake Maria na wana wao Arkadio na Yohana (karne ya 5-6)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
14Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo? Je, imani hiyo yaweza kumwokoa? 15Kama ndugu wa kiume au wa kike ni muhitaji wa mavazi au chakula cha kila siku, 16na mmoja wenu akawaambia, “Nendeni kwa amani, mkaote moto na mle vizuri,” lakini hamuwapi mahitaji muhimu ya mwili, hiyo yafaaa nini? 17Hali kadhalika, imani pekee, kama haina matendo, imekufa. 18Bado mtu fulani anaweza kusema, “ Una imani, na mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. 19Waamini kuwa kuna Mungu mmoja; uko sahihi. Lakini mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka. 20Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo isivyofaa? 21Je, si baba yetu Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo alipomtoa mwanawe Isaka juu ya madhabahu? 22Mnaona kuwa imani yake ilifanya kazi na matendo yake, na kwa matendo yake, imani yake ilifikia kusudio lake. 23Maandiko yalitimizwa yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na akahesabiwa kuwa ni mwenye haki.” Hivyo Abrahamu aliitwa rafiki wa Mungu. 24Mwaona kuwa kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu. 25Hali kadhalika, je, hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe na kuwapeleka kwa barabara nyingine? 26Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.
Injili
46Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara. 47Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” 48Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” 49Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, “Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita.” 50Akalitupa pembeni koti lake, akakimbia zaidi, na kuja kwa Yesu. 51Yesu akamjibu na kusema, “Unataka nikufanyie nini?” Yule mwanaume kipofu akamjibu, “Mwalimu, ninataka kuona.” 52Yesu akamwambia, “Nenda. Imani yako imekuponya.” Hapo hapo macho yake yakaona; na akamfuata Yesu barabarani.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Yohana (1938)
- Wafiadini Anania, padri, Petro, mlinzi wa gereza, na pamoja nao askari saba (295)
- Mtakatifu Mtawa Simeoni wa Kale (390)
- Askofu Mtakatifu Yusufu wa Studion, Askofu Mkuu wa Thesalonike, ndugu wa Mtakatifu Mtawa Theodoro wa Studion (830)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Theodoro, abati wa Studion (845)
- Mfalme Mwaminifu Daudi III Mjenzi Upya, mfalme wa Iberia na Abkhazia (1125)
- Mtakatifu Mtawa Ksenofoni wa Robeika (1262)
- Mtakatifu Mtawa Simeoni wa Kale
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 26 Januari katika kalenda ya kanisa ni 8 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki