Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 31 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 31 Desemba 2026
Alhamisi · Kipindi cha Noeli
Sikukuu na watakatifu
31 Desemba — Siku ya Saba katika Oktava ya Noeli
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Silvesta I, papa · Ukumbusho
Masomo ya siku
Somo la kwanza
18Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho. Kama ambavyo mmesikia kwamba mpinga kristo anakuja, hata sasa wapinga kristo wamekuja, kwa hali hii tunajua kwamba ni wakati wa mwisho. 19Walikwenda zao kutoka kwetu, kwani hawakuwa wa kwetu. Kama vile wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi. Lakini wakati walipo kwenda zao, hicho kilionyesha hawakuwa wa kwetu. 20Lakini mumetiwa mafuta na yule Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli. 21Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua na kwa sababu hakuna uongo wa ile kweli
Wimbo wa katikati
1Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote. 2Mwimbieni Yahwe, tukuzeni jina lake; tangazeni wokovu wake siku hadi siku. 11Mbingu na zifurahi, na nchi ishangilie; bahari na ivume na vyote viijazavyo vipige kelele kwa shangwe. 12Mashamba yashangilie na vyote vilivyomo. Kisha miti ya mstuni ipige kelele kwa furaha 13mbele za Yahwe, maana yeye anakuja. Anakuja kuihukumu nchi. Naye atauhukumu ulumwengu kwa haki na mataifa kwa uaminifu wake.
Injili
1Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. 2Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu. 3Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika. 4Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote. 5Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha. 6Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana. 7Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye. 8Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru 9Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja 10Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua. 11Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea. 12Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu, 13Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe. 14Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15Yohana alishuhudia kuhusu yeye, na alipaza sauti akisema, “Huyu ndiye ambaye nilisema habari zake nikisema, “Yule ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu amekuwako kabla yangu.” 16Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa. 17Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo. 18Hakuna mwanadamu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mtu pekee ambaye ni Mungu, aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane.
Watakatifu wa siku
- Mt. Silvesta I, papa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki