Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 31 Desemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 18 Desemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 31 Desemba 2026

Alhamisi · Wiki ya 31 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini Sebastiani na wenzake: Nikostrato (mtunza hazina), mke wake Zoe, Kastorio, Trankilino, padri, na wanawe Markelino na Marko, mashemasi, Klaudio, mkuu wa magereza, mwanawe Simforiano, ndugu yake Viktorino, Tiburtio na Kastulo (karibu 287 au 304)

Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Yak 1:19–27

19Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika, 20kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu. 21Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu. 22Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe. 23Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo. 24Hujitathimini uso wake, na huenda zake na baada ya muda mfupi husahau anavyofanana. 25Bali mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili, sheria ya uhuru, na kuendelea kuitii, si kwa sababu yeye ni msikilizaji anayesahau, huyu mtu atabarikiwa anapoitenda. 26Ikiwa mtu yeyote atafikiri mwenyewe kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, huudanganya moyo wake na dini yake ni bure. 27Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.

Injili

Mk 9:10–16

10Ndipo waliyatunza mambo wao wenyewe. Lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake “kufufuliwa kutoka kwa wafu” 11Walimwuliza Yesu,”Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?” 12Akawaambia, “hakika Eliya atakuja kwanza kuokoa vitu vyote. Kwa nini imeandikwa Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi na achukiwe? 13Lakini nasema kwenu Eliya alikwisha kuja, na walimfanya kama walivyopenda, kama vile maandiko yasemavyo kuhusu yeye.” 14Na waliporudi kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na Masadukayo walikuwa wanabishana nao. 15Na mara walipomwona, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia. 16Aliwauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao juu ya nini?”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 31 Desemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 18 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 31 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki