Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 1 Januari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 1 Januari 2027
Ijumaa · Kipindi cha Noeli
Sikukuu na watakatifu
Mt. Maria, Mama wa Mungu
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
22Tena BWANA akanena na Musa, akasema, 23“nena na Harunu na wanawe. Uwaambie, 'mtawabariki wana wa Israeli kwa njia hii. Mtawaambia, 24BWANA na awabariki na kuwatunza. 25BWANA na awaangazie nuru ya uso wake na awe mwenye neema kwenu. 26BWANA na awatazame kwa neema na awape amani.'” 27Ni kwa jinsi hii kwamba wanaweza kuwapa jina langu wana wa Israeli.”
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo. Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah 2ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. 4Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 5Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 7Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.
Somo la pili
4Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe, mzaliwa wa mwanamke, mzaliwa chini ya sheria. 5Alifanya hivi ili kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria, ili kwamba tupokee hali ya kuwa kama wana. 6Kwa sababu ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, “Abba, Baba.” 7Kwa sababu hii wewe si mtumwa tena bali mwana. Kama ni mwana, basi wewe pia ni mrithi kupitia Mungu.
Injili
16Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama. 17Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto. 18Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji. 19Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake. 20Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao. 21Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki