Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 25 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Novemba 2026
Jumatano · Wiki ya 26 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Yohana Mwenye Huruma, Patriarki wa Aleksandria (616-620)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
18Ninaliweka agizo hili mbele yako Timotheo, mtoto wangu. Nafanya hivi kulingana na unabii uliotolewa hapo kwanza kukuhusu wewe, ili kwamba uhusike katika vita njema. 19Fanya hivyo ili kwamba uwe na imani na dhamiri njema. Baadhi ya watu wameyakataa haya wakaangamiza imani. 20Kama vile Himeneyo na Alekizanda ambao nimempa shetani ili wafundishwe wasikufuru. 2:8Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka. 9Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa. 10Pia nataka wavae mavazi yanayowastahili wanawake wanaokiri uchaji kwa kupitia matendo mema. 11Mwanamke na ajifunze katika hali ya utulivu na kwa utii wote. 12Simruhusu mwanamke kufundisha, au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume bali aishi katika hali ya ukimya. 13Kwa kuwa Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. 14Adamu hakudanganywa, lakini mwanamke alidanganywa kabisa katika uasi. 15Hata hivyo, ataokolewa kwa kupitia kuzaa watoto, kama wataendelea katika imani na upendo na katika utakaso na akili njema.
Waraka (ya Alhamisi)
1Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema. 2Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi,, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe uwezo wa kufundisha. 3Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha. 4Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote. 5Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu? 6Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu. 7Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu. 8Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa. 9Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa. 10Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama. 11Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote. 12Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao. 13Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Injili
48Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi. 49Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka, 50Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika! 51Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko. 52Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu. 53Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake. 54Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa, 55Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa. 56Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo? 57Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo? 58Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani. 59Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.
Injili (ya Alhamisi)
1Kwa wakataihuo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao. 2Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo? 3Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo. 4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu? 5Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia. 6Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata. 7Akamwambia mtunza bustani, 'Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani ulete uharibifu wa ardhi? 8Mtunza bustani akajibu na kusema, 'uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake. 9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate.!”'
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Nilo, mfungaji (karne ya 5)
- Wafiadini wa Kikasisi Konstantino, Vladimir, Aleksanda, Mathayo, Demetrio, mapadri (1937)
- Mfiadini Boris (1942)
- Nabii Ahiya (960 K.K.)
- Mbarikiwa Yohana Mwenye Nywele Nyingi, mtenda miujiza wa Rostov (1580)
- Kupatikana kwa masalia ya Nilo, anayetoa manemane, wa Athos (1815)
- Mtakatifu Mtawa Nilo, anayetoa manemane, wa Athos († 1651)
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Mwenye Huruma”
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 25 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki