Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 20 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Novemba 2026
Ijumaa · Juma la 33 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 33 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
8Sauti niliyosikia kutoka mbinguni iliniambia tena: “Nenda, chukua gombo dogo lililofunuliwa ambalo kiko katika mkono wa malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.” 9Kisha nilikwenda kwa malaika na kumwambia anipe gombo dogo. Aliniambia, “Chukua gombo na ule. Litalifanya tumbo lako liwe na uchungu, lakini katika mdomo wako litakuwa tamu kama asali.” 10Nilichukua gombo dogo kutoka mkononi mwa malaika na kulila. Lilikuwa kitamu kama asali katika mdomo wangu, lakini baada ya kula, tumbo langu lilikuwa na uchungu. 11Kisha baadhi ya sauti ziliniambia, “Unapaswa kutabiri tena kuhusu watu wengi, mataifa, lugha, na wafalme.”
Wimbo wa katikati
Zab 119:14, 24, 72, 103, 111, 131
14Ninafurahi katika njia ya amri za agano lako zaidi kuliko katika utajiri. 24Amri za agano lako ni furaha yangu, na washauri wangu. 72Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. 103Ni jinsi gani maneno yako ni matamu kwenye majaribu yangu, naam, matamu kuliko asali kinywani mwangu! 111Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu. 131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
Injili
45Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza, 46akiwaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,' lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi”. 47Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua, 48lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki