Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 25 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Oktoba 2026
Jumapili · Juma la 30 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 30 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
21Hauta mkosea mgeni au kumnyanyasa, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. 22Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiye kuwa na baba. 23Ukiwadhuru ata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao. 24Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba. 25Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anaye kopesha hela kwake au kutoza faida. 26Ukichukuwa vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama, 27kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi, mtumishi wa Yahwe, alipomwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu katika ile siku ambayo Yahwe alimuokoa kutoka katika mkono wa adui zake wote na kutoka katika mkono wa Sauli. Yeye aliimba: Nakupenda, Yahwe, nguvu yangu. 2Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, yeye ambaye aniwekae kweye usalama; yeye ni Mungu wangu, mwamba wangu; ninapata kimbilio kwake. Yeye ni ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. 3Nitamuita Yahwe kwa sababu anastahili kusifiwa, na nitaokolewa kutoka kwa adui zangu. 46Yahwe anaishi; mwamba wangu usifiwe. Ainuliwe Mungu wa wokovu wangu. 50Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na yeye huonyesha uaminifu wa agano lake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na ukoo wake milele.
Somo la pili
5Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu. 6Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu. 7Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini. 8Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote. 9Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli. 10Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.
Injili
34Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja. 35Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu. 36“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?” 37Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza. 39Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. 40Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki