Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 24 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 24 Oktoba 2026
Jumamosi · Juma la 29 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 29 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Antoni Maria Klareti, askofu · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
7Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo. 8Ni kama maandiko yasemavyo: “Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu.” 9Ni nini maana ya, “Alipaa,” isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia? 10Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote. 11Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu. 12Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. 13Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo. 14Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka. 15Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo. 16Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
Wimbo wa katikati
1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! 3Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini! 4Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. 5Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
Injili
1Kwa wakataihuo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao. 2Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo? 3Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo. 4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu? 5Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia. 6Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata. 7Akamwambia mtunza bustani, 'Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani ulete uharibifu wa ardhi? 8Mtunza bustani akajibu na kusema, 'uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake. 9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate.!”'
Watakatifu wa siku
- Mt. Antoni Maria Klareti, askofu
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki