Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Wafalme wa Yuda

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Wafalme wa Yuda

Shemaya azuia vita

1 Fal 12:21–24 · 2 Nya 11:1–4

1 Wafalme

1 Fal 12:21–24

21Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akawakusanya wote wa nyumba ya Yuda na kabila la Benjamini; walichaguliwa wanaume wanajeshi 180,000 ili wapigane na nyumba ya Israeli, kwa lengo la kurudisha ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.

22Lakini neno la Mungu likamjia Shemaya, mtu wa Mungu; likisema,

23“Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na kwa nuymba yote ya Yuda na Benjamini, na kwa watu wote; uwaambie,

24“BWANA asema hivi, Usipigane wala kuwavamia ndugu zako watu wa Israeli. Kila mtu lazima arudi nyumbani kwake, kwa kuwa jambo hili nimelisababisha mimi.” Kwa hiyo wakalisikiliza neno la BWANA na wakrudi nyumbani kwa njia zao na wakalitii neno lake.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 11:1–4

1Rehoroboamu alipofiki Yerusalemu, akawakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, wanaume 180,000 walaiaochaguliwa amabao wliakuwa wanajeshi, kwa ajili ya kupigana dhiidi ya Israeli, ili kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu.

2Lakini neno la Yahwe likamjia Shemaya mtu wa Mungu, likisema,

3“Sema kwa Rehoboamu mwana wa Selemani, mfalme wa Yuda, na kwa Israeli kataika Yuda na Benyamaini,

4Yahwe anasema hivi, “Msivamie wala kufanya vita dhidi ya ndugu zako. Kila mmoja lazima arudi kwenye nyumba yake, kwa maana nimesababisha jambo hili kutokea.” Kwa hiyo wakayatii maneno ya Yahwe na kuacha kumvamia Yeroboamu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY