Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Wafalme wa Yuda
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Wafalme wa Yuda
Shishaki aushambulia Yerusalemu
1 Fal 14:25–28 · 2 Nya 12:9–11
1 Fal 14:25–2825Ilitokea wakati wa mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu wakati Shishaki akiwa mfalme wa Misri, akaja kinyume na Yerusalemu.
26Akaichukua hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya BWANA, na ile hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya Mfalme. Akachukua kila kitu; Pia alizichukua zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa ametengeneza.
27Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake na akazikabidhi kwa wakuu wa walinzi, ambao walilinda malango ya kuingia kwa mfalme.
28Na ikawa kila mfalme alipoingia kwenye nyumba ya BWANA, wale walinzi walizibeba na baadaye walizirudisha katika chumba cha walinzi.
2 Nya 12:9–119Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Selemani. Mfalme
10Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikoni mwa maamrijeshi wa walinzi, amabao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.
11Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY