18:13Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka.
18:14Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lachishi, akisema, “Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia”. Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu.
18:15Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya Yahwe na kawenye hazina nyumba ya mfalme.
18:16Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la Yahwe na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru.
18:17Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo.
18:18Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki
18:19Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: “Nini chanzo cha ujasiri wako?
18:20Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu?
18:21Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hicho ndicho Farao mfalme wa Misri kwa ymtu yeyote ambaye anayemtumainia.
18:22Lakini kama ukiniambia, 'Tunamwamini Yahwe Mungu watu; je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, 'Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu'?
18:23Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi elfu mbili, kama unaweza kuwatafuta kuwaendesha kwa ajili yao.
18:24Wanawezaje kumpinga hata nahodha mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi!
18:25Je nimesafiri kwenda huko juu bila Yahwe kupapigania hapa mahali na kupaharibu? Yahwe ameniambia, 'Ishambulie hii nchi na uiharibu.”'
18:26Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, “Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani.”
18:27Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, “Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kuwachukua kuongea haya maneno? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
18:28Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, “Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfale wa Ashuru.
18:29Mfalme asema, 'Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu.
18:30Msimwache Hezekia akawatumainisha katika Yahwe, akisema, “Yahwe atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.'”
18:31Msikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: 'Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe.
18:32Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa.' Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, 'Yahwe atatuokoa.'
18:33Je miungu yeyote ya watu inayewaokoa kutoka kwenye nchi ya mfalme wa Ashuru?
18:34Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu?
18:35Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje Yahwe akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?”
18:36Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, “Msimjibu.”
18:37Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.
19:1Ikawa kuhusu kwamba wakati Mfalme Hezekia aliposikia taazrifa zao, akararua mavazi yake, akavaa nguo za magunia, na kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
19:2Akamtuma Elkana, ambaye alikua msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna yule mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walikuwa wamefunikwa na nguo za magunia, kwenda kwa Isaya mwana wa Amozi, yule nabii.
19:3Wakamwambia, “Hezekia wakisema, 'siku hii ni siku ya mateso, shutuma, na fedheha, kwa kuwa wakati umewadia watoto kuzaliwa, lakini hakuna nguvu ili wazaliwe.
19:4Inaweza kuwa Yahwe Mungu wako atasikia maneno yote ya amiri jeshi mkuu, ambaye mfalme wa Ashuru bwana wake amemtuma kumkaidi Mungu aliye hai, naye atayakemea yale maneno ambayo Yahwe Mungu wako aliyasikia. Sasa inua maombi yako juu kwa ajili ya mabaki yaliyo bakia hapo.”'
19:5Hivyo watumishi wa mfalme Hezekia wakaja kwa Isaya,
19:6na Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu: 'Yahwe asema hivi, “Usiyaogope maneno ambayo uliyoyasikia, pamoja na kwamba watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.
19:7Tazama, nitaweka roho ndani yake, na yamkini atasikia taarifa na kurudi kwenye nchi yake mwenyewe. Nitamfanya aanguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe."”'
19:8Kisha amiri jeshi mkuu akarudi na kumkuta mfalme wa Ashuru akipigana dhidi ya Libna, kwa kuwa alisikia kwamba mfalme alikuwa ameenda kutoka Lakishi.
19:9Kisha Senakeribu akasikia kwamba Tirhaka mfalme wa Kushi na Misri alihamasisha kupigana dhidi yake, hivyo akatuma wajumbe tena kwa Hezekia pamoja na ujumbe:
19:10“Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda, 'Asikudanganye Mungu wako unayemwamini, kusema, “Yerusalemu haitawekwa kwenye mikono ya mikono ya mfalme wa Ashuru.”
19:11Tazama, umesikia kwamba wafalme wa Ashuru wamemaliza nchi zote kwa kuziharibu kabisa. Kwa hiyo je utaokoka?
19:12Je wale miungu wa mataifa wamewaokoa, mataifa ambao baba zangu waliyaharibu: Gozani, Harani, Resefu, na watu wa Edeni katika Telasari?
19:13Je yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaimu, wa Hena, na Iva?”'
19:14Hezekia akapokea hii barua kutoka wale wajumbe na kuisoma. Kisha akapanda hata kwenye nyumba ya Yahwe na kuukunjua mbele yake.
19:15Kisha Hezekia akaomba mbele ya Yahwe na kusema, “Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya makerubi, wewe ni Mungu wa pekee juu ya tawala zote za dunia. Uliyeziumba mbingu na nchi.
19:16Tega sikio lako, Yahwe, na usikie. Fungua macho yako, Yahwe, na tazama, na sikia maneno ya Senakeribu, ambayo ameyatuma kumdhihaki Mungu aliye hai.
19:17Ni kweli, Yahwe, wafalme wa Ashuru ameyaharibu mataifa na nchi zao.
19:18Wameiweka miungu yao kwenye moto, kwa kuwa hawakuwa miungu lakini ilikuwa kazi ya mikono ya watu, ilikuwa miti na mawe. Hivyo Waashuru wamewaharibu.
19:19Basi sasa, Yahwe Mungu wetu, tuokoe, nakusihi, kutoka kwenye nguvu zake, ili kwamba mamlaka zote za dunia zipate kujua yakwamba wewe, Yahwe, ndiye Mungu wa pekee.”
19:20Kisha Isaya mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, “Yahwe, Mungu wa Israeli asema, 'Kwasababu umeomba kwangu kuhusiana na Senakeribu mfalme wa Ashuru, nimekusikia.
19:21Hili ndilo neno ambalo Yahwe ameliongea kuhusu yeye: “Bikira binti Sayuni amekudharau na kukucheka kwa dharau. Binti wa Yerusalemu akatikisa kichwa juu yako.
19:22Je ni nani uliyemchokoza na kumtukana? Dhidi ya nani umeinua sauti yako na kuinua macho yako katika majivuno? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!
19:23Kupitia wajumbe wako wamemdharau Bwana, na kusema, 'Pamoja na wingi wa magari yangu ya farasi nimeenda juu ya vilele ya milima, hata juu ya kilele cha Lebanoni. Nitaikata mierezi mirefu na kuchagua miti ya mivinje huko. Nitaingia sehemu za makazi yake yaliyo mbali, msitu wake uzaao sana.
19:24Nimechimba visima na kunywa maji mageni. Nimekausha mito yote ya Misri chini ya soli ya miguu yangu.'
19:25Je hukusikia jinsi nilivyoagiza tangu zamani, na kuyafanya tangu siku za zamani? Sasa ninalileta kupita. Uko hapa kupunguza miji isiyoingilika kwenye rundo la maangamizi.
19:26Makazi yao, ya nguvu kidogo, imevunjwa vunjwa na aibu. Wamekuwa mimea katika shamba, majani ya kijani, majani juu kwenye dari au kwenye shamba, lililochomwa kabla halijakua.
19:27Lakini najua kuketi kwako chini, na kutoka kwako, kuingia kwako dhidi yangu.
19:28Kwasababu kiburi chako kimeyafikia masikio yangu, Nitaweka kulabu yangu kwenye pua yako, na hatamu yangu kwenye mdomo wako; nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.”
19:29Hii ndiyo itakuwa ishara kwako: Mwaka huu mtakula vitu viotavyo porini, na katika mwaka wa pili vile vikuavyo katika huo. Lakini katika mwaka wa tatu ni lazima mpande na kuvuna, kupanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
19:30Mabaki ya nyumba ya Yuda ambayo yataokoka yatachukua tena mizizi na kuzaa matunda.
19:31Kwa kuwa mabaki yatatoka Yerusalemu, kutoka Mlima Sayuni wenye kuokoka utakuja. Wivu wa Yahwe wa majeshi utafanya hivyo.
19:32Kwa hiyo Yahwe asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hatakuja kwenye huu mji wala kupiga mshale hapa. Wala hatakuja mbele yake na ngao au kujenga boma dhidi yake.
19:33Njia ile ile aliyoijia ndiyo njia atakayoondokea; hatoingia mji huu - hivi ndivyo asemavyo Yahwe.”
19:34Kwa maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”'
19:35Ikawa kuhusu usiku huo ambao malaika wa Yahwe alitoka na kuvamia kambi ya Waashuru, akawaua maaskari 185,000. Kisha watu wakaamka asubuhi na mapema, miili ya watu waliokuwa wamekufa ilikuwa imelala kila mahali.
19:36Hivyo Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka Israeli na kwenda nyumbani na kuishi katika Ninawi.
19:37Baadaye, alipokuwa akiabudu kwenye nyumba ya Nisroki mungu wake, watoto wake Adramaleki na Shareza wakamuua kwa upanga. Kisha wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Kisha Esarhodani mwanaye akawa mfalme katika mahali pake.