Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Kutoka Hezekia hadi Yosia

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Kutoka Hezekia hadi Yosia

Hezekia awa mfalme

2 Fal 18:1–3 · 2 Nya 29:1–2

2 Wafalme

2 Fal 18:1–3

1Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.

2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria.

3Alifanya yaliyo mema usoni pa Yahwe, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 29:1–2

1Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.

2Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY