Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi
Raba yatekwa
2 Sam 12:26–31 · 1 Nya 20:1–3
2 Sam 12:26–3126Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake.
27Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, “Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji.
28Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu.”
29Hivyo Daudi akalikusanya jeshi lote na kwenda Raba; akapigana nao na kuuteka.
30Daudi akachukua taji ya dhahabu kutoka katika kichwa cha mfalme wao iliyokuwa na uzito wa talanta, na ilikuwa na jiwe la thamani ndani yake. Taji ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Kisha akachukua nyara za mji kwa wingi.
31Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu
1 Nya 20:1–31Ikaja kuwa wakati wa mvua, kipindi wafalme uenda vitani, Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kusikitisha nchi ya Waamoni. Alienda na kuteka Raba. Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu alishambulia Raba na kuishinda.
2Daudi alichukuwa taji la mfalme wao kichwani mwake, na akagundua linauzito wa talanta moja ya dhahabu, na ndani yake kulikuwa na mawe ya thamani. Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi, na akaleta mali nyingi za mji.
3Aliwaleta watu walio kuwa ndani ya mji na kuwalazimisha wafanye kazi kwa msumeno na jembe na shoka. Daudi aliwataka watu wote wa mji kufanya kazi hii. Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY