Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi

Majitu ya Wafilisti

2 Sam 21:18–22 · 1 Nya 20:4–8

2 Samweli

2 Sam 21:18–22

18Ikawa baadaye kuwa na vita tena kati ya Wafilisti huko Gobu, wakati Sibekai Mhushathi alipomwua Safu, aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Warefai.

19Ikawa tena katika vita na Wafilisti huko Gobu, huyo Elhanani mwana wa Jari Mbethlehemu akamwua Goliathi Mgiti, ambaye fumo la mkuki wake lilikuwa kama mti wa mfumaji.

20Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai.

21Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.

22Hawa walikuwa wa uzao wa Warefai wa Gathi, waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake

1 Mambo ya Nyakati

1 Nya 20:4–8

4Ilikuwa baada ya haya kukawa na pambano huko Gezeri na Wafilisti. Sibekai Mhushathi akamua Sipai, mmoja wa uzao wa Refaimu, na wa Filisti wakazidiwa.

5Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.

6Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu.

7Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.

8Hawa walikuwa uzao wa Refaimu wa Gathi, na waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa wanajeshi wake.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY