Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi

Wafilisti washindwa katika bonde la Refaimu

2 Sam 5:17–25 · 1 Nya 14:8–17

2 Samweli

2 Sam 5:17–25

17Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.

18Basi Wafilisiti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.

19Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, “Je niwashambulie wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?” Yahwe akamwambia Daudi, “Washambulia, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya wafilisti.”

20Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.

21Wafilisiti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.

22Kisha wafilisiti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.

23Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.

24Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisiti.”

25Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomwamuru. Akawaua wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.

1 Mambo ya Nyakati

1 Nya 14:8–17

8Sasa tangu Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo nae akaenda nje kinyume nao.

9Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.

10Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “ Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”

11Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “ Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.

12Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.

13Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.

14Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “ Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.

15Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”

16Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.

17Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY