Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Wafalme wa Yuda

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Wafalme wa Yuda

Athalia na mtoto Yoashi

2 Fal 11:1–21 · 2 Nya 22:10–12; 23:1–21

2 Wafalme

2 Fal 11:1–21

1Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.

2Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.

3Alikuwa pamoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya Yahwe, kwa mda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.

4Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta maamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya Yahwe. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya Yahwe. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.

5Akawaamuru, akisema, “Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,

6na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi.”

7Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya mfalme.

8Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.

9Hivyo mamia ya maamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.

10Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa maamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe.

11Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.

12Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpatia mikataba ya agano. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, “Mfalme na aishi!”

13Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya Yahwe.

14Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na manahodha na wapiga mabaragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”

15Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza maamri jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, “Mtoeni kwenye safu.” Atakayemfuata, muueni kwa upanga.” Kwa kuwa kuhani alisema, “Msimwache auawe kwenye nyumba ya Yahwe.”

16Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.

17Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Yahwe na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa Yahwe, na pia kati ya mfalme na watu.

18Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuingusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la Yahwe.

19Yehoyada akawachukua maamiri jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.

20Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.

21Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 22:10–12; 23:1–21

22:10Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaoana kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akaianuka na kuwauwa watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.

22:11Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuuwa.

22:12Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.

23:1Katika mwaka wa sa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.

23:2Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.

23:3Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, “Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.

23:4Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.

23:5Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.

23:6Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaoatumika. Wao wanaweza kuingia kwa sababu inawahusu.

23:7Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje.”

23:8Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana

23:9Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.

23:10Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.

23:11Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, “Aishi maisha marefu mfalme.”

23:12Athalia aliposikia kele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.

23:13na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!”

23:14Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, “Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga.” kwa maana kuhani alikwishasema, “Msimuue katika nyumba ya Yahwe.”

23:15Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.

23:16kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.

23:17Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.

23:18Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.

23:19Yehoyada akaweka walinzi katika malango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.

23:20Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme.

23:21Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY