Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Kuwahukumu wengine

Mt 7:1–5 · Lk 6:37–42

Mathayo

Mt 7:1–5

1Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.

2Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.

3Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?

4Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?

5Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.

Luka

Lk 6:37–42

37Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.

38Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”

39Kisha akawaambia mfano pia. “Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?

40Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.

41Na kwa nini basi wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti lililo ndani ya jicho lako huliangalii?

42Utawezaje kumwambia ndugu yako, 'Ndugu, naomba nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,' nawe huangalii boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza itoe boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY