Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Galilaya

Injili kando kwa kando · Katika Galilaya

Mtu mwenye jeshi la pepo

Mt 8:28–34 · Mk 5:1–20 · Lk 8:26–39

Mathayo

Mt 8:28–34

28Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.

29Tazama, walipaza sauti na kusema, “Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?”

30Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa,

31pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. “Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe.”

32Yesu akawaambia, “Nendeni!” Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.

33Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, hususani kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo.

34Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.

Marko

Mk 5:1–20

1Walikuja mpaka upande mwingine wa bahari, katika mkoa wa Gerasi

2Na ghafla wakati Yesu alipokuwa akitoka nje ya mtumbwi, mtu mwenye roho chafu alikuja kwake kutoka makaburini.

3Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia zaidi, hakuna hata kwa minyororo.

4Alikuwa amefungwa nyakati nyingi kwa pingu na minyororo. Aliikata minyororo na pingu zake zilivunjwa. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.

5Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata yeye mwenyewe kwa mawe makali.

6Alipomwona Yesu kwa mbali, alikimbilia kwake na kuinama mbele yake.

7Alilia kwa sauti kuu, “Wataka nikufanyie nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Ninakusihi kwa Mungu mwenyewe, usinitese.”

8Kwa kuwa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu.”

9Naye alimwuliza, “Jina lako ni nani?” Naye alimjibu, “Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi.”

10Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.

11Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likilishwa juu ya kilima,

12nao walimsihi, wakisema, “Tutume kwa nguruwe; tuingie ndani yao.”

13Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.

14Na wale waliokuwa wakiwalisha nguruwe walikimbia na kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na katika nchi. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.

15Ndipo walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyepagawa na pepo—aliyekuwa na Jeshi—amekaa chini, amevikwa, na akiwa katika akili yake timamu, nao waliogopa.

16Wale waliokuwa wameona kilichotokea kwa mtu aliyekuwa amepagawa na pepo waliwaambia kilichotokea kwake na pia kuhusu nguruwe.

17Nao walianza kumsihi aondoke katika mkoa wao.

18Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.

19Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, “Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alikufanyia Bwana, na rehema aliyokupa.”

20Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.

Luka

Lk 8:26–39

26Wakafika kwenye mji wa Gerasini iliyo upande wa nyuma ya Galilaya.

27Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.

28Alipomwona Yesu akalia kwa sauti, na akaanguka chini mbele yake. kwa sauti kubwa akisema, Nimefanya nini kwako, Yesu mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, Usiniadhibu mimi”

29Yesu akaamuru roho chafu imtoke mtu yule, kwa kuwa mara nyingi amepamgaa. hata kama alikuwa amefungwa minyororo na kubanwa na kuwekwa chini ya ulinzi, alivunja vifungo na kuendeshwa na mapepo mpaka jangwani.

30Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” akajibu akisema, “Legioni” Kwa maana mapepo mengi yameingia kwake.

31Wakaendelea kumsihi usituamuru twende kwenye shimo.

32Kundi la Nguruwe lilikuwa likichunga juu ya kilima, wakamsihi awaruhusu wakaingie kwa hao nguruwe. Na akawaruhusu kufanya hivyo.

33kwa hiyo wale mapepo wakamtoka mtu yule na kuingia kwa wale nguruwe, na lile kundi likakimbia kwenye mwinuko wa mlima mpaka ziwani na wakazama humo.

34wale watu waliokuwa wanachunga wale nguruwe walipoona kilichotokea, wakakimbia na wakatoa taarifa pale mjini na nje katika miji iliyowazunguka.

35Watu waliposikia hayo walienda kuona kilichotokea, na wakaja kwa Yesu na wakamwona mtu ambaye mapepo yalikuwa yamemtoka. alikuwa amevaa vizuri na mwenye akili timamu, amekaa kwenye miguu ya Yesu, na waliogopa.

36ndipo mmoja wao aliyeona kilichotokea alianza kuwasimlia wengine jinsi huyu mtu aliyekuwa anaongozwa na mapepo alivyoponywa.

37Watu wote wa mkoa wa Wagerasi na maeneo yaliyozunguka walimwomba Yesu aondoke kwao kwa sababu walikuwa na hofu kuu. Na aliingia kwenye mtumbwi ili arudi.

38Mtu yule aliyetokwa na pepo alimsihi Yesu kwenda naye, lakini Yesu alimwambia aende na kusema,

39“Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY