Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Njiani kwenda Yerusalemu

Injili kando kwa kando · Njiani kwenda Yerusalemu

Yesu awabariki watoto

Mt 19:13–15 · Mk 10:13–16 · Lk 18:15–17

Mathayo

Mt 19:13–15

13Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea.

14Bali Yesu akasema, “Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.

15Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.

Marko

Mk 10:13–16

13Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.

14Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.

15Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.

16Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.

Luka

Lk 18:15–17

15Watu walimletea watoto wao wachanga, ili aweze kuwagusa, lakini wanafunzi wake walipoona hayo, wakawazuia.

16Lakini Yesu akawaita kwake akisema, 'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie. Maana ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao.

17Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto ni dhahiri hatauingia. '

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY