Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Yesu amshukuru Baba

Mt 11:25–27 · Lk 10:21–22

Mathayo

Mt 11:25–27

25Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.

26Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.

27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.

Luka

Lk 10:21–22

21Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”

22“Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY