Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Warumi 12:19

Mstari wa Biblia · ULB

Warumi 12:19

Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”

Soma sura nzima: Warumi 12

Katika muktadha

16Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe.

17Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote.

18Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.

19Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”

20“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.”

21Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

Warumi 12

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleRomans 12:19Do not avenge yourselves, beloved, but leave room for God’s wrath. For it is written: “Vengeance is Mine; I will repay, says the Lord.”

Nukuu kutoka Agano la Kale

Kum 32:35Kisasi ni changu kutoa, na fidia, katika muda mguu wao utakapotereza; kwa maana siku ya maafa kwao ipo karibu, na vitu vitakavyokuja juu yao vitaharakisha kutendeka.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Ebr 10:30Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa”. Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake”.
Mit 24:29Usiseme, “ Mimi nitamtendea kile alichonitendea; nitalipiza kwa kile alichofanya.”
Mit 20:22Usiseme “ Mimi nitakulipiza kwa kosa hili” Msubiri Yehova na yeye atakuokoa.
1 The 4:6Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia.
Rum 12:14Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.
Law 19:18Usijilipize kisasi au kuwa na chuki yoyote dhidi ya mtu yeyote wa watu wako, lakini badala yake mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Yahweh.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki