Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Yohana 15:7

Mstari wa Biblia · ULB

Yohana 15:7

Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.

Soma sura nzima: Yohana 15

Katika muktadha

4Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu.

5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.

6Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.

7Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.

8Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.

9Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.

10Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.

Yohana 15

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleJohn 15:7If you remain in Me and My words remain in you, ask whatever you wish, and it will be done for you.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Zab 37:4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
1 Yoh 5:14Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia.
Yn 14:13Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
1 Yoh 3:22Na chochote tuombacho tutakipokea kutoka kwake, kwa sababu tunazishika amri zake na tunafanya mambo yanayopendeza mbele zake.
Yn 15:16Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
Mt 7:7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
Yn 16:23Siku hiyo hamtaniuliza maswali. Amin, Amin, nawaambia, Mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu.
Gal 5:16Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki