Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Kutoka 20:12
Mstari wa Biblia · ULB
Kutoka 20:12
Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.
Katika muktadha
9lazima ufanye kazi zako zote kwa siku sita.
10Ila siku ya saba ni Sabato kwaajili ya Yahweh Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, au mwana wako, au binti yako, au mtumishi wako wakiume, au mtumishi wako mwanamke, au ng'ombe zako, au mgeni aliye ndani ya malango yako.
11Kwa siku sita Yahweh aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na siku ya saba alipumzika. Kwa hiyo Yahweh aliibariki siku ya Sabato na kuitenga.
12Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.
13Usiue.
14Usifanye uasherati (usizini).
15Usiibe kwa mtu yoyote.
Kwa Kiingereza
Honor your father and mother, so that your days may be long in the land that the LORD your God is giving you.Imenukuliwa katika Agano Jipya
Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.'“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi), “ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.”Kwa kuwa Musa alisema, 'mheshimu baba yako na mama yako,' na 'Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa.'Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'.”Unazijua amri- usizini, usiue, Usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki. “Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi), “ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.Mheshimu baba yako na mama yako, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru kufanya, ili kwamba uweze kuishi muda mrefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako akupa, ili kwamba iende kwa uzuri kwako.Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee. Inunue kweli, lakini usiiuze; nunua hekima, nidhamu, na ufahamu. Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia. Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako; zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki