Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 1 Timotheo 4:8

Mstari wa Biblia · ULB

1 Timotheo 4:8

Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.

Soma sura nzima: 1 Timotheo 4

Katika muktadha

5Kwa sababu kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi.

6Kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu, utakuwa mtumishi mzuri wa Yesu Kristo. Kwa sababu umestawishwa kwa maneno ya imani na kwa mafundisho mazuri ambayo umeyafuata.

7Lakini zikatae hadithi za kidunia ambazo zinapendwa na wanawake wazee. Badala yake, jifunze mwenyewe katika utaua.

8Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.

9Ujumbe huu ni wakuaminiwa na unastahili kukubaliwa kabisa.

10Kwa kuwa ni kwa sababu hii tunataabika na kufanya kazi kwa bidii sana. Kwa kuwa tunao ujasiri katika Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, lakini hasa kwa waaminio.

11Uyaseme na kuyafundisha mambo haya.

1 Timotheo 4

Kwa Kiingereza

Berean Standard Bible1 Timothy 4:8For physical exercise is of limited value, but godliness is valuable in every way, holding promise for the present life and for the one to come.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mt 6:33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
1 Tim 6:6Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
Zab 37:3–4Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani. Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
Mit 19:23Kumheshimu Yehova huwaelekeza watu kwenye uzima; mwenye nayo atashibishwa na hatadhurika kwa madhara.
Mit 22:4Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Yehova ni utajiri, heshima na uzima.
Kol 2:21–23“Msishike, wala kuonja, wala kugusa”? Haya yote yameamuriwa kwa ajili ya uharibifu ujao na matumizi, kutokana na maelekezo na mafundisho ya wanadamu. Sheria hizi zina hekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili. Lakini hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili.
Zab 37:11Lakini wapole watairithi nchi nao watafurahia katika mafanikio makubwa.
Mk 10:30ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki