Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 29 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Desemba 2027
Jumatano · Kipindi cha Noeli
Sikukuu na watakatifu
29 Desemba — Siku ya Tano katika Oktava ya Noeli
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Thoma Becket, askofu na shahidi · Ukumbusho
Masomo ya siku
Somo la kwanza
3Kwa hili twajua kwamba twamjua yeye, kama tukizitunza amri zake. 4Yeye asemaye, “Namjua Mungu,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake. 5Lakini yeyote ashikaye neno lake, kweli katika mtu yule upendo wa Mungu umekamilishwa. Katika hili twajua kwamba tuko ndani yake. 6Yeye asemaye anaishi ndani ya Mungu anapaswa mwenyewe pia kuenenda kama vile Yesu Kristo alivyoenenda. 7Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani ambayo mmekwisha kuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno ambalo mlilolisikia. 8Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya, ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu, kwa sababu giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza 9Yeye asemeye yuko kwenye nuru na amchukia ndugu yake yuko katika giza hata sasa. 10Yeye ampendaye ndugu yake anaishi katika nuru na hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza. 11Lakini yeye amchukiaye ndugu yake yuko gizani na anatembea gizani; Yeye hajui wapi aendako, kwa sababu giza limeyapofusha macho yake.
Wimbo wa katikati
1Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote. 2Mwimbieni Yahwe, tukuzeni jina lake; tangazeni wokovu wake siku hadi siku. 3Tangazeni utukufu wake kati ya mataifa, matendo yake ya ajabu kati ya mataifa. 5Maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, bali ni Yahwe aliye zifanya mbingu. 6Heshima na adhama ziko mbele zake. Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
Injili
22zao zilizotakiwa za utakaso zilipopita, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana. 23Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.” 24Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.” 25Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana. 27Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria, 28ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema, 29“Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako. 30Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako, 31ambao umeonekana kwa macho ya watu wote. 32Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo kwa Wamataifa na utukufu wa watu Israeli.” 33Baba na Mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake. 34Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga. 35Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike”.
Watakatifu wa siku
- Mt. Thoma Becket, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki