Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 28 Desemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Desemba 2027

Jumanne · Kipindi cha Noeli

Sikukuu na watakatifu

Watoto Watakatifu Wasio na Hatia, mashahidi

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 Yoh 1:5–2:2

5Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia: Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo. 6Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli. 7Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambi zote. 8Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu. 9Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu. 2:1Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki. 2Yeye ni mpatanishi kwa dhambi zetu, na si kwa dhambi zetu pekee, lakini pia kwa ulimwengu mzima.

Wimbo wa katikati

Zab 124:2–5, 7–8

2“Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu, 3basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu. 4Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia. 5Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.” 7Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka. 8Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.

Injili

Mt 2:13–18

13Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, “Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize. 14Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri. 15Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, “Kutoka Misri nimemwita mwanangu.” 16Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi. 17Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia, 18“Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 28 Desemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki