Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 29 Desemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Desemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Desemba 2027

Jumatano · Wiki ya 28 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2

Sikukuu na watakatifu

Nabii Hagai (500 K.K.)

Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana

Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 Tim 4:9–22

9Jitahidi kuja kwagu haraka. 10Kwa kuwa Dema ameniacha. Anaupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia, na Tito alikwenda Dalmatia. 11Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko uje naye kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma. 12Nimemtuma Tikiko Efeso. 13Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi. 14Alekizanda mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. 15Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu. 16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia. 17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba. 18Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amen 19Msalimie Priska, Akila na nyumba ya Onesiforo. 20Erasto alibaki huko Korintho, lakini Trifimo nilimuacha Mileto akiwa mgonjwa. 21Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote. 22Mungu awe pamoja na roho yako, Neema iwe nawe.

Injili

Mk 8:30–34

30Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye. 31Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na viongozi na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka. 32Alisema haya kwa uwazi. Ndipo Petro akamchukua pembeni na akaanza kumkemea. 33Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na akamkemea Petro na kusema, “Pita nyuma yangu Shetani! Hujali mambo ya Mungu, isipokuwa mambo ya watu.” 34Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, “Kama kuna mtu anataka kunifuata, ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake, na anifuate.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 29 Desemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 29 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki