Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 17 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Novemba 2027

Jumatano · Juma la 33 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Elizabeti wa Hungaria, mtawa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 17:1, 5–6, 8, 15

1Maombi ya Daudi. Sikia ombi langu kwa ajili ya haki, Yawhe; uusikilize mwito wangu wa msaada. Uyasikilize maombi yangu yatokayo katika midomo isiyo na udanganyifu. 5Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza. 6Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea. 8Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako 15Bali mimi, nitauona uso wako katika haki; Nitashuhudiwa, pale nitakapo amka, na macho yako.

Injili

Lk 19:11–28

11Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja. 12Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi. 13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.' 14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.' 15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara. 16Wa kwanza akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. ' 17Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. ' 18Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.' 19Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.' 20Na mwingine akaja, akasema, 'Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa, 21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. ' 22Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda. 23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida? 24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.' 25Wakamwambia, 'Bwana, yeye ana mafungu kumi. ' 26'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. 27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. '' 28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 17 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki